Header Ads

KATAVI: ASHIKILIWA NA POLICE KWA UBAKAJI NA ULAWITI

 KATAVI MKULIMA ABAKA NA KULAWITI BINT WA MIAKA MITANO  SABABU YA USHIRIKIANA


Summary: "uchunguzi wa awali imebainika kuwa tukio hili linahusiana na imani za kishirikina kwani mtuhumiwa aliahidiwa kulipwa ng'ombe mara tuu baada ya..." ACP Makame.

Katavi: Jeshi la police mkoa wa katavi linamshikilia mkulima mmoja mkoani humo katika wilaya ya Tanganyika kwa tuhuma za ubakaji na ulawiti wa bint mdogo umri wa miaka mitano .

Kamanda wa police mkoa wa katavi ACP Ali Hamad  Makame amewaambia waandishi wa habari kuwa tukio hilo limetokea tareh 13/05/2022 ambapo mtuhumiwa anadaiwa kumvizia bint huyo njiani na kumkamata kisha kutekeleza kitendo chake kwenye vichaka vilivyo karibu na njia .

"Uchunguzi wa awali imebainika kuwa tukio hili linahusiana na imani za kishirikina, kwani mtuhumiwa aliahidiwa kulipwa ng'ombe mara tuu baada ya kutekeleza kitendo hicho na kwamba mara baada ya kutekeleza kitendo hicho aende kumuoshea shambani kwake ili iwe kama sehemu ya uzindikaji wa shamba " Alisema ACP Makame.

No comments

Note: only a member of this blog may post a comment.

Powered by Blogger.