Header Ads

NGUO ZA SHANGAZI KAJA: DIAMOND PLATNUMZ AJA KIVINGINE

                 DIAMOND PLATNUMZ 




               Photo: Diamond platnumz 

Msanii wa muziki wa bongofleva nchini Tanzania Diamond platnumz kupitia ukurasa wake wa instagram ameweza kuwaonyesha mashabiki wake na wadau wote wa sanaa ya mziki duniani  vazi lenye muonekano wa kushangaza .

Vazi hilo lilitotengenezwa kwa kutumia mifuko ya kubebea mizigo maarufu kama shangazi kaja limewashangaza wengi juu ya ni ipi sababu ya diamond platnumz kuvaa hivyo . 

Hata hivyo diamond platnumz hakuweka wazi ni nani designer wa vazi hilo na lipi lengo la yeye kuvaa vazi hilo . 

Wiki kadhaa zilizopita msanii mwingine wa muziki wa kizazi kipya Tanzania (Bongofleva) Harmonize alishika hatamu kwenye mitandao ya kijamii baada ya kuvaa sketi. Hata hivyo huu ni mfululizo wa matukio ya wasanii kuvaa mavazi ya mfano huu kutangaza sanaa yao na ubunifu. 

    "  Sanaa ni ubunifu na ubunifu ni kufanya kitu ambacho wengine hawakifanyi " 

Unalipa alama ngapi vazi hili la diamond platnumz?

No comments

Note: only a member of this blog may post a comment.

Powered by Blogger.