MHE . JUMAA AWESO KUTAFUTA UFUMBUZI KERO YA MAJI MADANGA
KATA YA MADANGA WILAYANI PANGANI
Summary: Akizingumza kwa njia ya simu mbunge wa jimbo la pangani Mhe: Jumaa Aweso amesema kuwa swala la maji ni moja ya ahadi zake alizowaahidi wananchi hivyo ataendelea kupigania kuhakikisha kuwa huduma ya maji safi na salama inapatikana wakati wote.
Serikali iko mbioni kutatua kero ya maji kwa wananchi wa kata ya Madanga wilayani Pangani Mkoani Tanga baada ya mradi uliokuwepo hapo awali kukauka, hali inayopelekea wakazi wa kata kufuata maji katika taasisi za kidini ikiwemo misikitini.
Akizingumza kwa njia ya simu mbunge wa jimbo la pangani Mhe Jumaa Aweso amesema kuwa suala la maji ni moja ya ahadi zake alizowaahidi wananchi hivyo ataendelea kupigania kuhakikisha kuwa huduma ya maji safi na salama inapatikana wakati wote.
Mhe Jumaa Aweso amesema kuwa serikali imeshatenga kiasi cha pesa za kitanzania shilingi bilioni moja kutoa huduma ya maji katika kijiji cha boza na kuipeleka katika kata ya Madanga wilayani Pangani kutokana na eneo hilo visima kukauka.
Hata hivyo Mhe Jumaa Aweso ameongeza kuwa mradi huo utaanza kutekelezwa katika mwaka mpya wa fedha mnamo mwezi July na inatarajiwa mradi huo kuja na suluhu ya kudumu.
Post a Comment