Header Ads

MWENGE WA UHURU NDANI YA MKOA WA MANYARA

 WAPOKELEWA 13/06/2022 KILELE 19/06 


Summary: Ndani ya mkoa wa Manyara utakimbizwa katika halmashauri saba za mkoa huo na kutembelea miradi 39 ya maendeleo yenye thamani ya bilioni 23.2 

Mwenge wa uhuru jana tarehe 13/06/2022 umepokelewa katika mkoa wa Manyara ukitokea mkoani Kilimanjaro na kilele chake kinatarajiwa kuwa june 19.

Mwenge wa uhuru ndani ya mkoa wa Manyara utakimbizwa katika halmashauri saba za mkoa huo na kutembelea miradi 39 ya maendeleo yenye thamani ya bilioni 23.2 za kitanzania. Huku miradi 17 yenye thamani ya shilingi bilioni 20.7 itawekewa mawe ya msingi, miradi ya bilioni 1.6 itafunguliwa na miradi tisa yenye thamani ya shilingi 843.7 million itatembelewa.

Hata hivyo katika mkoa wa Manyara mwenge utakimbizwa katika mamlaka ya serikali za mitaa ambazo ni Simanjiro , Kiteto , Babati mji , Babati wilaya , Hanang , Mbulu wilaya na Mbulu mji.

Charles Makongoro Nyerere ( RC) ameahidi kusimamia vyema shughuli za mwenge wa uhuru kipindi chote utakapokuwa mkoani mwake .

                 Fm Manyara 

No comments

Note: only a member of this blog may post a comment.

Powered by Blogger.