Header Ads

MWANDISHI WA HABARI APOTEA MSITU WA AMAZON

                RIO DE JENEIRO : BRAZIL 


Rio de janeiro: Brazil; Mwandishi wa habari mkongwe raia wa uingereza Dom Philips inaripotiwa kuwa amepotea katika msitu wa amazon. Habari zinaeleza kuwa Dom Philips akiwa na mwenyeji wake Bruno A. Pereira (Mtaalam wa misitu ) nchini Brazil wote wamepotea katika msitu wa amazon msitu ambao ni mkubwa zaidi duniani.


Taarifa za kupotea kwao zinakuja baada ya kupoteza mawasiliano ya satellite kwa muda wa saa 30 tangu walipoingia katika msitu mnene wa amazon, msitu wenye viumbe hatari pamoja na mito mingi. 

 Mke wa Dom Philips ameendelea kuomba msaada na kuweka msisitizo kuwa itakuwa salama kwake kama mume wake atapatikana itakuwa vigumu kwake kuishi bila ya uwepo wa mume wake kipenzi.  Dom philips mwandishi wa habari mahiri na mwandishi nguli wa vitabu mpaka kupotea kwake bado alikuwa katika majukumu yake ya kikazi akiwa kama freelancer wa maswala ya habari . The Guardian inatambua mchango wake.

No comments

Note: only a member of this blog may post a comment.

Powered by Blogger.