20 Wafa Ajalini Nigeria

WATU 20 WAFIA AJALINI ABUJA NIGERIA 

Ajali mbaya nchini Nigeria

ABUJA NIGERIA:  Mamlaka ya Serikali Nigeria imethibitisha kuwa takribani watu 20 mwishoni mwa juma wamefariki kutokana na ajali mbili kubwa za barabarani zinazohusisha lori. Mamlaka inasema kuwa moja ya ajali hizo ni lori lililokuwa limebeba kontena lenye urefu wa mita 12 sawa na futi 39 lilipokuwa linapita darajani dereva alishindwa kulimudu na kisha kugongana na basi lililokuwa linapakiza abiria . 
Kontena hilo lilianguka kwenye basi na kisha kuwaponda abiria . Miongoni mwa waliofariki ni wanaume watano , wanawake wawili na watoto wawili .

Aidha mamlaka ya usimamizi usalama barabarani jimbo la Lagos ( Lastma ) ameripoti kuwa jumapili iliokoa watu wanne (04) katika ajali nyingine baada ya saa za operesheni huko Ojuelegba Kusini Magharibi mwa jimbo la Lagos. Katibu mkuu wa Lastma Olufeni Osanyintolu amesema " Tumekamilisha shughuli , Tuliweka maiti kwenye chumba cha kuhifadhia na majeruhi alikimbizwa hospital ambako anapatiwa matibabu ya uhakika . Tunaangalia kiujumla na tunafanya uchunguzi " . 

 

Next Post Previous Post
sr7themes.eu.org