Fahamu haya Kuhusu Mbuga Na Hifadhi Za Taifa La Zambia
FAHAMU KUHUSU MBUGA NA HIFADHI ZA WANYAMAPORI NCHINI ZAMBIA
Leo February 02 , 2023 unasogezewa habari za Hifadhi Za Taifa La Zambia, Kweny kipindi cha Cities story . Lengo ni ufahamu mengi zaidi kuhusu habari za miji na majiji.
Nchi Zambia ya Zambia iliyopo katika bara la Africa imesheheni wingi wa rasilimali ikiwemo hifadhi za kitaifa na mbuga, vitu vinavyoifanya nchi ya Zambia kuwa na nafasi nzuri katika shughuli za utalii. Kitu kinachoongeza pato la Taifa la Zambia.
Fahamu mbuga na Hifadhi hizo kwa undani kama ifuatavyo hapa hapa .
1. Mbuga ya Kitaifa ya Blue Lagoon; Mbuga iliyopo umbali wa kilomita 120 magharibi mwa mji wa Lusaka, mbuga hii hata hivyo ipo upande wa kaskazini mwa mto kafule .
Ukweli ni kwamba changamoto kubwa katika mbuga ya Blue Lagoon ni mafuriko , ni mara chache kuona watalii katika mbuga hii kutokana na miondombinu mibovu na finyu pamoja na ugumu wa kuifikia mbuga hii.
2. Mbuga Ya Isangano ; Mwaka 1972 hifadhi hii ilianzishwa, ikiwa na ukubwa wa eneo lenye kilomita 840 mashariki mwa ziwa bangweulu . Bado mafuriko kipindi cha mvua kubwa ni changamoto inayoikabili hifadhi ya Isangano , Hata hivyo uchache wa wanyamapori ni changamoto nyingine inayopelekea uchache wa wageni katika mbuga .
3. Hifadhi ya Kitaifa ya Kafue - Mojawapo ya mbuga kubwa zaidi za kitaifa ulimwenguni, Kafue National Park ilianzishwa mnamo 1924 na inajulikana sana ulimwenguni kote kwa idadi yake ya wanyama ya kushangaza
4. Hifadhi ya Lavushi Manda ; Ni Hifadhi yenye mandhari nzuri sana na yenye kuvutia pia . Kilele cha mlima Lavushi chenye urefu wa mita 1800 na maporomoko ya maji huipamba zaidi Hifadhi hii, Hifadhi ya Lavushi ni maarufu zaidi kutokana na uwepo wa wingi wa ndege wanaovutia kwa sauti na rangi zao .
Aidha inaripotiwa kuwa idadi ya wanyama katika Hifadhi hii imeanza kupungua katika siku za hivi karibuni. Wageni katika Hifadhi hii hufurahia sana kupanda mlima , kufanya matembezi na kuvua samaki .
5. Hifadhi ya Liuwa Plain ; Zaidi ya Karne moja wanyamapori wamekuwa wakiishi katika Hifadhi hii asilia . Hapo mwanzo eneo hili lilitumiwa kama pori la mawindo ya mfaulme wa Lozi , lakini sasa hivi ni moja ya Hifadhi yenye kuvutia zaidi . wageni katika Hifadhi hii hushuhudia kundi kubwa la nyumbu na uhamaji wao .
Chanzo Kafunta Safaris
Ni matumaini kuwa umefahamu kitu leo katika Cities story session hapa Modealer

