Nchini Tanzania Watumiaji Wa Simu Za Mkononi Watakiwa Kuhakiki usajili wa Sim Card Zao
NCHINI TANZANIA WATUMIAJI WA SIMU ZA MKONONI WATAKIWA KUFANYA UHAKIKI WA USAJILI WA SIM CARD ZAO .
Tanzania : Watumiaji wa Simu Za Mkononi na sim card za mitandao mbalimbali ya simu Nchini Tanzania wanatakiwa kufanya uhakika wa usajili wa simu card zao mara moja kabla ya mwezi February .
Mapema January 24 , Waziri wa Teknolojia ya habari na mawasiliano Nchini Tanzania Nape Nnauye amewataka wamiliki wa Simu card Nchini Tanzania kufanya uhakika wa usajili wa Sim Card kabla ya mwezi February, Aidha inaelezwa kuwa wale watakaokwenda kinyume na agizo simu card zao zitazimwa mara moja bila kuonewa huruma yeyote ile.
Watumiaji wa Simu card Nchini Tanzania wameshauriwa kukamilisha uhakiki huo kupitia simu zao za Mkononi au kufika katika maduka ya mitandao husika ya simu Card zao wanazotumia, ikiwa ni pamoja na Tigo, Ttcl, Airtel, Vodacom na Halotel .
Tarehe 13/2/2023 saa kumi jioni kama kutakuwa na laini ambayo haijahakikiwa ndio itakuwa mwisho wa kutumika kwake,hakuna nyongeza ya muda, wale ambao hawajahakiki kuhakiki ni rahisi sana unaingia mwenyewe kwenye simu yako unahakiki unakuwa umemaliza"_Waziri Nape Nnauye
