Watu tisa wafa 30 Kujeruhiwa ajali ya gari Katavi
Watu tisa wafa 30 Kujeruhiwa ajali ya gari wilaya Ya Tanganyika Mkoani Katavi .
Basi la Komba's linalofanya Safari zake kutoka Kigoma Mpanda Mkoa wa Katavi limepata ajali mbaya kwenye mlima wa Nkondwe uliopo Wilaya ya Tanganyika .
Taarifa iliyotolewa na Mkuu wa Mkoa wa katavi kutokana na ajali iliyotokea Watu 9 Wamefariki dunia na wengine 30 wamejeruhiwa na majeruhi wanaendelea na matibabu kwenye hosipitali ya Majalila , Mpanda na Rufaa Katavi.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Katavi, Ali Makame amesema ajali hiyo ilitokea Alasiri ya Machi 6, 2023 ikihusisha basi kampuni ya Komba’s. Ameeleza kuwa baada ya kufika katika mlima huo gari liliserereka na kudondokea kwenye bonde kubwa lenye kina cha mita zisizopungua 75.

