Burdock Mmea Unaoaminiwa Kutibu Saratani

Burdock Mmea Unaoaminiwa Kutibu Saratani Na Maradhi Mengine Mengi .

Burdock Plant Roots

Dunia yetu imejaa idadi kubwa ya miti, mimea na maua, kwaujumla miti, mimea na maua yanayotuzunguka ni dawa ya maradhi sugu yanayotusumbua kwa miongo kadhaa .

Katika chapisho hili leo unasogezewa mmea huu uitwao burdock, mmea ambao unaaminiwa kuwa ni silaha katika mapambano dhidi ya maradhi sugu ikiwemo saratani na mengine mengi.  

         Asili ya mmea wa burdock 

Mmea wa burdock asili yake inatajwa kuwa ni bara la Asia, Europe na America. Katika nchi zilizopo katika mabara tajwa mmea huu si mgeni kwa raia wa nchi hizo , ni mmea maarufu na umekuwa ukitumika katika matumizi ya kila siku, yaani katika nyakati za asubuhi (kinywaji) mchana ( mboga) na hata usiku .   

Mmea wa burdock katika matumizi yake huweza kuandaliwa na kutumika kama mafuta, mboga na pia kama chai yaani kinywaji , hata hivyo katika jamii za watu wa china mzizi wa mmea huu hutumika sana katika mambo ya dawa za kitamaduni .

Tafiti iliyofanywa na Sciencedirect mwaka 2016 imeweka wazi juu ya faida ya mmea huu katika uwanja wa utabibu ( tiba ) ya maradhi sugu. Japokuwa mpaka sasa hakuna tafifi zilizofanywa za sehemu moja moja za mmea huu yaani majani, mizizi, maua na shina kubainisha faida za kila sehemu ya mmea huu , tafiti zote zilizofanywa ni tafiti za jumla katika mmea. 

          Maradhi gani burdock hutibu ?  

- Saratani ( breast cancer) 

- Maradhi ya ini  ( Liver cancer ) 

- Maradhi ya moyo na kisukari ( pressure and diabetes ) 

- Maradhi ya figo ( Kidney failure) 

- Uchujaji wa sumu mwilini 

- Kurekebisha kiwango cha maji mwilini 

         Vipi utanufaika na mmea huu ? 

Kunufaika na mmea wa burdock, siri pekee ni matumizi ya kila siku. Matumizi ya mmea huu huanzia katika maandalizi. Baadhi ya watumiaji wa Asia, Europe na America hukausha na kisha kutumia kama chai , wengine hutumia majani ya mmea huu kuchemsha na kunywa kama supu au huchanganya na mboga zingine na kupika pamoja. Hata hivyo baadhi ya watumiaji husaga mzizi wa mmea huu na kupata unga na kisha kutumia. 

Inaelezwa kuwa kila kilichopo katika mmea huu ni tiba katika afya ya binaadamu dhidi ya maradhi sugu yanayotusumbua kila siku. 

Jee matumizi ya burdock yanayo madhara kwa binaadamu yeyote ? 

Hakuna madhara ya moja kwa moja yaliyoidhinishwa kutokana na matumizi ya burdock mpaka sasa, ila inaelezwa kuwa kwa baadhi ya watu hairuhusiwi kwao kutumia mmea huu katika kipindi fulani . Mfano wajawazito ni hatari kwao kutumia mmea huu kwani huleta athari katika uterus na hatimae hupelekea premature babies . 

Dunia imejaa wingi wa mimea ambayo ni dawa na tiba katika maradhi sugu yanayotusumbua endelea kuwa nasi kwa habari nyingi za afya na dondoo za tiba . 




Next Post Previous Post
sr7themes.eu.org