Makki Ki Roti Chapati Za Unga Wa Mahindi

Unazifahamu Chapati Za Unga Wa Mahindi. 

Modealer Daily News

Unafahamu chochote kuhusu uwepo wa chapati za unga wa mahindi? kama jibu ndio au hapana basi leo kutana na hii habari kuhusu chapati hizo.

Ni maarufu kwa jina la Makki Ki Roti, ni chapati tamu sana na kamwe huwezi kumwambia kitu  mhindi wa Punjabi kuhusu chapati hizi na akakuelewa hata kidogo. 

Huko India baadhi ya watu hutumia sana chapati hizi kama sehemu ya mlo wa muda wowote haswa asubuhi au jioni , huandaliwa kwa namna ya tofauti kidogo na chapati zile za unga wa ngano peke yake na kisha katika uchomaji wake ni sawasawa na uchomaji wa chapati za kawaida.

Katika kukoleza ladha ya ulaji wengine hupenda kuweka asali kidogo pembeni huku wengine wakisakata chapati hizi kwa sharubati tamu kabisa. Upishi ni sanaa na sanaa hii tangu enzi na enzi imekuwepo katika dunia . Ni tofauti ndogo sana iliyopo kati ya jamii moja na nyingine juu ya upishi wa aina fulani ya chakula na kipi ni sahihi kuliwa katika jamii husika. 

Jee unatamani siku moja nawe upike chapati hizi? basi fanya hivyo na kisha utualike .