Katazo La Kutembea Na Sime, Fimbo, Na Rungu Kwa Wamaasai Visiwani Zanzibar.
Mhe: Rashid Msaraka mkuu wa wilaya ya mjini Magharibi ametamka wazi juu ya katazo la jamii ya wamaasai visiwani Zanzibar kutembea hadharani wakiwa na sime, fimbo au marungu kwani hizo ni silaha za jadi na wanamotembea sio msituni hivyo sio mahali pake.
Aidha katazo hilo linakuja kufuatia uwepo wa habari kuwa kuna vijana wa kimaasai ambao walimshambulia kwa silaha zao za jadi mfanyakazi mmoja wa halmashauri ( mlinzi) baada ya uwepo wa operesheni ndogo ya hamisha hamisha wafanyabiashara katika maeneo ya milki ya barabara katika eneo la mji mkongwe.
Video zinazosambaa mitandaoni zinamuonesha Rashid Msaraka akiwahoji vijana wa kimaasai kuwa iwapo walisikia tukio walilofanya wenzao na kisha ndio akatamka katazo hilo. Jee unalo la kusema? basi tuandikie maoni yako katika kurasa zetu za mitandao ya kijamii au wasiliana nasi kwa barua pepe.