Waislam Wasiofunga Wakamatwa Nigeria
Nigeria: Police wa kiislam wa Hisbah nchini Nigeria kwa mujibu wa Islamic Shariah wamewakamata watu wapatao kumi na moja na kutishia kukamata wengine zaidi kwa kosa la kula katika mwezi mtukufu wa Ramadhan.
Mwezi mtukufu wa Ramadhan ni mwezi ambao waumini wa dini tukufu ya kiislam wanajizuilia kula na kunywa na yote yenye kufunguza tangu mapambazuko hadi machweo ya jua majira ya magharibi.
Aidha katika tukio hilo la watu kumi na moja kukamatwa, inaripotiwa kuwa baadhi yao walikamatwa maeneo ya sokoni na kituo cha mabasi baada ya kukutwa wakila ndani ya mchana wa mwezi wa Ramadhan.
Hata hivyo baadhi ya waumini wa dini nyingine zisizokuwa uislam nchini Nigeria , wanaharakati na wakosoaji wamepinga kitendo hicho kilichofanywa na askari wa kiislam wa Hisbah cha kuwakamata watu hao. Waumini wa dini ya kiislam duniani kote wanaendelea na mfungo wa mwezi wa Ramadhan ulioanza siku mbili zilizopita na kumalizika baada ya siku 29 au 30 za mfungo.