Waziri Wa Mambo Ya Nje Kuwakamata Raia Wake Wanaojihusisha Kijeshi Na Israel.
South Africa: Wizara ya mambo ya nje ya nchini South Africa imetangaza mpango wake wa kuwakamata raia wake ambao wanajihusisha na maswala ya kijeshi na nchi ya Israel.
Bi Naledi Pandor waziri wa mambo ya nje South Africa amesema kuwa tayari ametoa maelezo yenye maagizo ya tahadhari kwa wote wenye uraia wa South Africa na wanapigana vita upande wa Israel kuwa watakaporejea nchini South Africa watakamatwa.
" When you come home, we are going to arrest you, I have already issued a statement alerting those who hold South Africa citizenship and are fighting alongside or in the Israel Defense Forces.
South Africa imekuwa ni nchi iliyopo katika mstari wa mbele kulaani na kuikosoa Israel kwa mauaji ya raia huko Gaza hata kufikia hatua Rais wa South Africa Cyril Ramaphosa kuiburuza mahakamani Israel kwa kushirikiana na viongozi wengine pamoja na wanaharakati wa nchini South Africa na nje ya mipaka ya nchi hiyo.