Habari: Rais wa France Emmanuel Macron ameingilia kati vita ya Russia na Ukraine na kutangaza waziwazi kuwa France ipo tayari kuisaidia Ukraine kushinda vita yake dhidi ya Vladimir Putin wa Russia.
Akizungumza na waandishi wa vyombo mbalimbali vya habari Emmanuel Macron ametamka kauli kadhaa ambazo zinaashiria nia yake ya kweli ya kutaka kuiunga mkono Ukraine kushinda vita yake dhidi ya Russia.
Emmanuel Macron amesema kuwa kamwe hakutakuwa na amani hadi Ukraine Ishinde Vita na kurudisha maeneo yake yaliyochukuliwa na Russia ikiwemo eneo muhimu la Crimea.
Hata hivyo Macron ameongeza kwa kusema kuwa ushindi wa Russia dhidi ya Ukraine ni anguko la thamani ya bara la ulaya na umoja wa ulaya ( European Union ) . " Russian Victory against Ukraine will reduce Europe's Credibility to zero " , " There would no peace untill Ukraine win the war and return it's occupied areas including Crimea" Emmanuel Macron.
Bado vita ya Russia na Ukraine ni jambo gumu ambalo haifahamiki kuwa lini litamalizika kutokana na kila mmoja kutunisha misuli dhidi ya mengine huku washirika wanaomuunga mkono Ukraine wakiingilia kati kwa kutoa msaada wa kijeshi ikiwemo silaha, huku Russia chini ya Rais Vladimir Putin ikiongeza nguvu yake mbali na kuwekewa vikwazo vya kiuchumi.
Kwa upande wa jicho la chambuzi za kisiasa na maswala ya Geopolitics inaonekana kuwa Ukraine hapiganii maslahi yake tuu bali maslahi ya kundi kubwa la nchi za ulaya hivyo swala la Vita hii kumalizika ni gumu.