Kisindo Kesi Ya Tundu Antipas Lissu Mahakamani Dar es salaam Leo

Kishindo Kesi Ya Tundu Antipas Lissu Mahakamani Jijini Dar es salaam Leo . 

Tundu Antipas Lissu Mahakamani

Picha: Mwenyekiti chama cha demokrasia na maendeleo ( Chadema) ndani ya ukumbi wa mahakama Jijini Dar es salaam 6/10/25. 

Habari: Jijini Dar es salaam, mwenyekiti wa chama cha demokrasia na maendeleo ( Chadema) Tundu Antipas Lissu mapema leo hii jumatatu ya tarehe 06/10/2025 amefikishwa katika ukumbi wa mahakama kuu masjala ndogo jijini Dar es salaam kuendelea na shauri la mashtaka na kesi ya uhaini inayomkabili. 

Aidha habari kutoka mahakamani zinaeleza kuwa kesi hiyo itasikilizwa mfululizo kuanzia leo hii mpaka hapo October 24 mwaka 2025. Kutoka viwanja vya mahakamani ulinzi na usalama vimeimarishwa huku kesi ikiendelea. 

Hata hivyo Lissu ameingia ndani ya viwanja vya mahakama akiwa na furaha, hamu na shauku ya kutaka kujua nini hatma yake . Tundu Antipas Lissu anakabiliwa na kesi ya uhaini kwa kufanya uchochezi wa kutaka kuzuia uchaguzi mkuu kutofanyika na mengine yamfano huu . Upande wa Jamhuri unawakilishwa na mawakili wake wa utetezi huku Tundu Antipas Lissu akijiwakilisha yeye mwenyewe tuu. 




Next Post Previous Post
sr7themes.eu.org