Ngumi Hewani Tundu Antipas Lissu Mahakamani Dar es salaam Leo
Tundu Antipas Lissu Akiwasili Mahakamani Dar es salaam Leo Ngumi Ikiwa Hewani.
Pichani ni Mwenyekiti chama cha demokrasia na maendeleo ( Chadema) Tundu Antipas Lissu akiwasili ndani ya ukumbi wa mahakama kuu masjala ndogo jijini Dar es salaam huku akipunga mkono wa ngumi hewani mbele ya maafisa wa jeshi la magereza na mawakili wa Jamhuri.
Tundu Antipas Lissu amefikishwa mahakamani kuendelea na shauri la kesi ya uhaini inayomkabili. Kesi ambayo itaendelea kusikilizwa mfululizo hadi mnamo October 24 , 2025. Kesi ya Tundu Antipas Lissu inatajwa kuwa kesi muhimu sana yenye kufuatiliwa na halaiki ya watu duniani kote.
Ni kesi yenye mvuto mkubwa katika uwanja wa sheria , ambapo watu mbalimbali wamekuwa wakiifatilia tangu kuanza kwake mpaka hapa ilipofikia huku wageni mbalimbali wa kitaifa na kimataifa wakizidisha kiu ya kutaka kujua ni ipi hatma ya Tundu Antipas Lissu juu ya kesi hii inayomkabili dhidi ya Jamhuri Ya Muungano Wa Tanzania .
