FAHAMU HISTORY YA KIWANDA CHA VOLKSWAGEN UJERUMANI
Sehemu ya kwanza
VOLKSWAGEN. Maana yake Gari la Wananchi
Makazi makuu yapo mjini Wolfsburg katika jimbo la Saksonia . Hata hivyo kiwanda Cha volkswagen huzalisha na kutengeneza magari mengine kama vile Bugatti, Lamborghini, skoda , Seat , audi na scania .
Kiwanda Cha volkswagen kilianzishwa mwaka 1937 . Baada ya aliyekuwa Kiongozi wa nchi ya Ujerumani wakati huo Adolf Hitler alipotaka gari nzuri ya bei nafuu ambayo kila muajiriwa wa kipato Cha chini angemudu kununua .
Ndio muhandisi Ferdinand Porsche alipoombwa kuunda gari la Bei nafuu . Umbo la mwanzo la gari alilounda lilisababisha gari kuitwa Kafer .
Kipindi Cha mwaka 1939 mwanzoni kabisa kabla ya vita vya pili vya dunia kuanza, kiwanda kipya kilijengwa karibu zaidi na maeneo ya mashambani . Katika eneo linaloitwa Wolfsburg eneo maarufu hii leo .
Hitaji la magari ya kijeshi na vita kwaajili ya kuendesha vita kiwanda kilibadili muundo wa magari waliyokuwa wakiunda na kuanza kutengeneza magari ya kijeshi.
Baada ya Ujerumani kushindwa katika vita kiwanda Cha volkswagen kiliwekwa chini ya himaya ya waingereza kabla ya mambo kubadilika hapo baadae.
Tukutane sehemu ya pili wiki ijayo .
http://www.volkswagen.com/.
Post a Comment