Ajali ya basi la sheraton watu saba wafa
Watu saba wafariki ajali ya basi la sheraton Mkoani geita .
Geita: Kaimu Kamanda wa Polisi mkoa wa Geita, Kamishina Msaidizi wa Polisi (ACP) Berthaneema Mlay amethibitisha kutokea kwa ajali iliyosababisha vifo vya watu saba huku wengine zaidi ya kumi wakijeruhiwa .
Ni katika ajali ya basi la abiria kampuni ya Sheraton lenye namba za usajili T922 ADC iliyotokea katika kijiji cha Mwilima kata ya Kasamwa mkoani Geita tarehe 07/03/2023.
