Haya ndio madhara ya kula chumvi nyingi

Madhara ya kula chumvi nyingi katika afya 

Madhara ya kula chumvi nyingi

Chumvi ( munyu ) ni kiungo muhimu katika upishi, chumvi huongeza ladha na kuongeza madini joto katika mwili wa binaadamu lakini hata hivyo baadhi ya chumvi huongeza madini chuma na kumlinda mtumiaji na maradhi ya rovu ( goiter ) .  

Tafiti mbalimbali zimefanywa kubaini madhara ya kula chumvi nyingi katika afya ya binaadamu , moja ya tafiti hizo ni hii iliyofanywa na kuchapishwa na Harvard Education and nutrition sources . Tafiti ambayo imebaini madhara mengi ya utumiaji wa chumvi nyingi haswa chumvi zenye wingi sodium chloride . Kabla ya kuangazia katika madhara hayo ni muhimu ukafahamu ya kuwa ukiachana na chumvi inayotumika jikoni / mezani ( table salt) kuna aina zaidi ya saba za chumvi chapisho litakalofuata litaangazia juu ya aina hizo . 

 Ni madhara gani ya kula chumvi nyingi? 

- Maradhi ya moyo ( pressure, moyo kuvimba , moyo kuuma na shida katik aorta).

- Maradhi ya figo ( Kidney failure ) 

- Matatizo ya kibofu cha mkojo ; hii hutokana na kufeli kwa figo katika uchujaji wa mkojo vizuri . 

Health line katika chapisho lao lenye data juu ya madhara ya kula chumvi nyingi, wanataja madhara ya muda mfupi ya kula chumvi nyingi ambayo ni kama vile ;- 

- Kupoteza maji mengi mwilini kwa njia ya jasho na kukojoa sana.

- Kukojoa mkojo wenye harufu kali na rangi chafu .

-Kuongezeka kwa harufu mbaya ya jasho . NB madhara ya muda mfupi yanaweza kuwa dalili za kugundua iwapo mwili wako una chumvi nyingi.

Nini ufanye unapogundua kuwa umekula chumvi nyingi au mwili wako una chumvi nyingi ?  

Tafiti mbalimbali zilizofanywa zimeweka wazi chakufanya pale mtu anapogundua kuwa amekula chumvi nyingi au mwili wake una chumvi nyingi sana. Miongoni mwa mambo ya kufanya ni pamoja na kuzidisha kula matunda yenye potassium, mboga za majani kwa wingi, kunywa maji mengi na kuongeza unywaji wa maziwa.  Hata hivyo njia salama zaidi ni kuacha kula chumvi nyingi. 


Next Post Previous Post
sr7themes.eu.org