Kumbukizi Kifo Cha Magufuli Tulipotoka Na Tulipo Sasa Bila Uwepo Wa John Magufuli.
Ni miaka mitatu imefika sasa tangu kifo cha aliyewahi kuwa Rais wa tano Jamhuri ya muungano wa Tanzania Hayati John Pombe Magufuli. Kifo cha hayati magufuli kamwe hakiwezi kusahaulika vichwani mwa watu wa Tanzania, Afrika Mashariki, Afrika bara na hata dunia kwa ujumla. Misimamo mikali vita juu ya ufisadi, rushwa na matumizi mabaya ya madaraka ni miongoni mwa mambo muhimu ambayo uongozi wa Magufuli ulizingatia.
Leo March 17 2024 ni kumbukumbu ya kifo cha Hayati John Pombe Magufuli kuna mengi sana ya kukumbuka, kutafakari na kufahamu kama raia wa nchi yenye muelekeo imara wenye dira ya maendeleo. kipindi cha utawala wa John Magufuli dunia nzima imeshuhudia Taifa la Tanzania likiingia katika uchumi wa kati kutoka katika hali mbaya hadi kufikia hali nzuri ya kimaendeleo iliyokwenda sambamba na maendeleo ya sekta ya mawasiliano na uchukuzi .
Magufuli aliwezaje? ni swali gumu kujibu kubwa na jepesi kwa wasiotafakari vyema, ni ukweli usiofichika kuwa Magufuli anastahili heshima kubwa, hakuna mkamilifu zaidi ya Mwenyezi Mungu tuu hivyo ni wazi kuwa Magufuli zipo sehemu na nyakati fulani alitetereka kama binaadamu ila hapa anastahili pongezi nyingi. Mirada mikubwa ya maendeleo aliyoifanya ndani ya muda mfupi tena kwa mkopo mdogo aliochukua kwa kipindi cha miaka yake mitano ya kwanza apewe pongezi.
Magufuli bus terminal: ni mradi mkubwa sana wa kimaendeleo ambao magufuli aliukamilisha, kujenga kituo kikubwa cha mabasi ya kusafirisha abiria mbezi haikuwa kazi rahisi, ni kazi ngumu yenye kuhitaji usimamizi wa karibu, muda na akili imara ya kizalendo. Magufuli amekamilisha na dunia imeshuhudia.
Kijazi Interchange: Nao ni mradi mwingine wa kimkakati wa kimaendeleo ambao John Pombe Magufuli alihakikisha anaukamilisha mara baada ya kuanza kwake, hata hivyo haikuwa rahisi kwa nchi ya Tanzania tuliyoaminishwa kuwa ni masikini siku zote kukamilisha mradi huu mkubwa.
Standard Gauge ( SGA ): mradi wa ujenzi wa railway ya kisasa sio kazi rahisi lakini Rais Magufuli kwa uzalendo wake alihakikisha anauanzisha na anaukamilisha japokuwa mpaka kifo kinamkuta alibakisha sehemu chache ya kukamilika kwa mradi. Jee Magufuli pesa alipata wapi ndani ya muda mchache?
Bwawa la kufua umeme la Julius Nyerere: Ni mradi mkubwa nao uliolenga kuondoa adha na kero ya kukatika kwa umeme bila mpangilio nchini Tanzania, ni miongoni mwa miradi mikubwa ya maendeleo barani Africa ambao ulishangaza dunia na viongozi mbalimbali hata kutaka kumjua huyu Magufuli ni nani .
Kwa kifupi tuu hiyo ni miradi michache aliyoifanya John Pombe Magufuli ndani ya muda mfupi, lakini kwa upande wa mambo ya kijamii Magufuli alikuwa ni mfariji mkuu wa Taifa, mtia moyo na hamasa katika kila gumu , vita dhidi ya coronavirus ( uviko 19 ) ilipambanua vyema uwezo wa Magufuli wa kutia hamasa na kufariji. Ni kipindi hiki kigumu ambacho raia wa mataifa mengi walitamani na wao wangekuwa watanzania baada ya viongozi wao kuingia mkenge wa kuweka katazo la watu kwenda kazini.
Ni katika kipindi cha utawala wa Magufuli aspect ya uchumi wa nchi ya Tanzania ilionekana ikikuwa kwa kasi huku heshima katika matumizi ya fedha za umma ikiwa juu zaidi , rushwa na matumizi mabaya ya fedha za umma vikitokomea mbali sana.
Jee misingi ya demokrasia ilikuwaje? Unapoizungumzia demokrasia unajumuisha vitu kama vile uhuru wa kujieleza ( freedom of speech ) , uchaguzi huru ( free and fair election), uwazi ( transparency ) , accountability na mengine ya muhimu. Kama ilivyoandikwa hapo juu kuwa kama binaadamu kuna maeneo Magufuli alikosea sababu hakuna mkamilifu, swala la kuzuia mikutano ya vyama vya upinzani, kukosekana kwa uhuru wa kujieleza kupitia vyombo vya habari kwa kiasi kikubwa ni kwenda kinyume na misingi ya demokrasia.
Sakata la mwaandishi wa habari za kiuchunguzi Erick Kabendera kuswekwa rumande hata kuzuiwa kushiriki mazishi ya mama yake mzazi kuliichafua serikali ya Rais Magufuli katika upande wa demokrasia, sakata la aliyewahi kuwa mbunge Tundu Lissu kushambuliwa kwa risasi kisha kuporwa ubunge na kukosa stahiki zake ni jambo jingine.
Katika uwajibikaji serikali ya Rais Magufuli imewajibika haswa kuanzia ngazi za juu hadi ngazi za chini za utumishi na uongozi hata kupatikana kwa msemo wa " hapa kazi tuu " . Magufuli aliishi ilani ya chama chake kwa kutimiza ahadi zake nyingi wakati wa kampeni za kuwania kiti cha Urais. " Watu wa mkuzi muheza tanga nichagueni niwe Rais wenu niwaletee maendeleo ya kweli, kuna watu wachache pale Dar es Salaam ndio wanaokula pesa zenu na kuzorotesha maendeleo, mkinichagua nitaanza nao " . Magufuli aliyasema hayo Kijiji cha mkuzi muheza akiwa anaelekea wilayani Pangani.
Tulipo sasa hali ikoje chini ya Samia? Baada ya kifo cha Rais Magufuli, mazishi yake na taratibu zote kukamilika aliyekuwa makamu wa Rais yaani Samia Suluhu Hassan rasmi alikamata kiti cha kuwa Rais wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania.
Nini alifanya Rais Samia Suluhu Hassan baada ya kukamata madaraka? Kwanza kuunda baraza lake la mawaziri huku Mhe Kassim Majaliwa akimuacha kuendelea kuwa waziri mkuu wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania kutokana na kutekeleza vyema majukumu yake . Pili rais Samia Suluhu Hassan alirudisha misingi ya demokrasia nchini Tanzania kuanzia kwenye mahakama na vyombo vingine vya serikali hata kufikia hatua wale waliokuwa mafichoni, ughaibuni kurejea nchini.
Usimamizi na kuendeleza miradi iliyoachwa na Magufuli; chini ya uongozi wa Rais Samia Suluhu Hassan serikali imeendelea na usimamizi wa miradi ya kimaendeleo iliyoachwa na Magufuli ikiwemo SGA, Bwawa la kufua umeme la Julius Nyerere, wami bridge, kigongo - busisi bridge na mingine mingi.
Kuruhusu maandamano ya amani; hili ni jambo kubwa la kidemokrasia nchini Tanzania, Rais Samia Suluhu Hassan chini ya uongozi wake vyama pinzani vimepata nguvu ya kusema, kukosoa bila woga na hata kusikilizwa kwa kina na yakinifu. Dunia imeshuhudia na inashuhudia wimbi la maandamano ya vyama vya upinzani CHADEMA huku mikutano ya vyama vya upinzani ikirudi kwa kasi chini ya utawala wa Rais Samia Suluhu Hassan. Kipindi cha magufuli nani angeandamana?
Ni mengi ambayo utawala wa Rais Samia umefanya na bado unaendelea kufanya huku changamoto za kibinaadamu zikiwa hazikosekani lakini lipo jambo la kujiuliza kwa pamoja juu ya ongezeko kubwa la deni la Taifa hili lililokuwa katika uchumi wa kati, kupanda kwa gharama za maisha na jee kodi zilizopo zinaweza kufanya hali kuwa bora zaidi au kuwa mbaya zaidi ?